Wananchi watakiwa kuwa watulivu kufuatia utabiri wa hali ya hewa
20 September 2023, 4:59 pm
Katika mikoa iliyotajwa inapaswa kuchukua tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa mwaka huu mkoa wa Katavi haujaainishwa.
Na John Benjamin – Katavi
Wananchi mkoani Katavi wametakiwa kuwa watulivu kufuatia kutolewa kwa taarifa ya utabiri wa hali ya hewa ukionyesha baadhi ya mikoa kuwa na kiwango kikubwa cha mvua
Imebainisha kuwa mvua za vuli zinatarajiwa kuanza mwezi Oktoba hadi Desemba 2023 katika maeneo yanayopata mvua za msimu miwili kwa mwaka.
Akizungumza na mpanda redio fm meneja wa mamlaka ya hali hewa mkoa wa Katavi Juma Hamis Binda amesema kuwa katika mikoa iliyotajwa inapaswa kuchukua tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa mwaka huu huku mkoa wa Katavi haujaainishwa.
Aidha Binda ameleeza kuwa mikoa ambayo imetajwa kuwa na kiwango kikubwa cha mvua ni ile mikoa ambayo ipo karibu na ziwa Victoria na Bahari ya hindi ambapo amefafanua kuwa Taarifa ya utabiri ya mwelekeo wa mvua za vuli 2023 iliyotolewa na mamlaka ya hali ya hewa Tanzania tarehe 24 mwezi wa 8 mwaka huu imebainisha kuwa mvua za vuli zinatarajiwa kuanza mwezi Oktoba hadi Desemba 2023 katika maeneo yanayopata mvua za msimu miwili kwa mwaka.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo mvua zitakuwa za juu ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi ya mikoa ya Kagera,Geita,Mwanza,Shinyanga,kusini mwa mkoa wa Simiyu Pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma,Dar es salaam Tanga,Pwani,ikiwemo visiwa vya Mafia na kaskazini mwa mkoa wa Morogoro.