Waandishi wa habari nyanda za juu kusini wanufaika na mafunzo ya Tadio
12 September 2023, 7:27 am
Mafunzo haya yatawasaidia waandishi wa habari kuwa na uelewa zaidi kidigital kwa kuchapisha Habari ,Makala na kufikisha elimu mbalimmbali kupitia radio tadio
Na Anna Millanzi – Mbeya
Waandishi wa Habari wa radio jamii nyanda za juu kusini wamepatiwa mafunzo ili kufanya kazi zao kwa weledi na kutumia fursa Iliyopo kwa kuendana na teknolojia.
lengo la mafunzo hayo ni kuwafundisha namna ya kuandaa na kusambaza habari zao kupitia teknolojia kwa njia ya mtandao na kuwainua kichumi kwa kutumia mitandao.
Mafunzo hayo yamewakutanisha Wahariri Pamoja na Waandishi wa habari kutoka vituo vya radio tisa ukanda wa Nyanda za juu kusini ili kuwajengea uwezo .
Akizungumza mara baada ya kutolewa mafunzo hayo Afisa miradi Saumu Bakari wa mtandao wa radio jamii Tanzania (TADIO)amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwafundisha namna ya kuandaa na kusambaza habari zao kupitia teknolojia kwa njia ya mtandao na kuwainua kichumi kwa kutumia mitandao.
Mwezeshaji Wa mafunzo hayo Amua Rushita ameeleza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia waandishi wa habari kuwa na uelewa zaidi kidigital kwa kuchapisha Habari,Makala na kufikisha elimu mbalimmbali kupitia radio tadio.
Baadhi ya waandishi wa habari katika mafunzo hayo wamesema mafunzo hayo yanatija kwao kwani yanakwenda kubadilisha mitazamo na kuongeza fursa kuifikia jamii na kuongeza uchumi wa radio.