Wanafunzi 6000 Mpanda wataraji kuhitimu darasa la saba
11 September 2023, 7:54 am
MPANDA
Zaidi ya Wanafunzi 6000 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba Manispaa ya Mpanda katika Mtihani Unaotarajiwa kufanyika Sept 13 na 14 mwaka 2023.
Akizungumza na Mpanda Radio fm Afisa Elimu Shule za Msingi Manispaa ya Mpanda Godfrey Kalulu amesema kuwa mtihani unategemewa kufanyika nchi nzima na kuwataka wazazi kutengeneza mazingira ya kuwaandaa watoto kwa maisha baada ya kumaliza elimu ya msingi ikiwemo maandalizi ya elimu ya upili.
Aidha Wakazi wa Manispaa ya Mpanda Wakizungumza wamewaomba wazazi wenye Watoto wanaotarajiwa kufanya mtihani huo kuendelea kusimamia malezi bora kuelekea kwenye mtihani na baada ya kuhitimu ili kuwatengenezea mwelekeo mzuri wa maisha.
Kwa Mujibu wa Afisa Elimu shule za Msingi watahiniwa kutoka katika Manispaa ya Mpanda 6639 kutoka katika shule 45 za msingi wanatarajiwa kufanya mtihani huo ambapo wasichana ni 3498 na wavulana wakiwa ni 3141.