Mpanda FM

NIshati ya Mafuta Yawa Kikwazo cha Uchumi

6 September 2023, 10:10 am

MPANDA

Nishati ya mafuta ya petrol imetajwa kuwa ni Moja ya sababu inayorudisha nyuma uchumi katika halmashauri ya manispaa ya mpanda mkoani hapa.

Wakizungumza na Mpanda redio FM watumiaji wa vyombo vya moto wamesema kuwa wamekuwa wakitumia muda Mwingi kupanga foleni kwa ajili ya kupata nishati hiyo bila ya mafanikio yoyote.

Kaimu katibu tawala msaidizi, msimamizi wa maswala ya uchumi na uzalishaji mkoa wa Katavi Neimia James amefanya ukaguzi kwa baadhi ya vituo vya mafuta na kuamuru vituo vilivyo na mafuta kutoa Huduma na kuwaomba wananchi kuwa watulivu katika kipindi ambacho serikali inaendelea kufanyia kazi changamoto hiyo

Changamoto ya upatikani wa nishati ya mafuta katika mkoa wa katavi imekuwa ni ya kujirudiarudia licha ya serikali kuendelea kufanya jitihada ya kutatua changamoto hiyo.

#mpandaradiofm97.0

#Ewura