Madiwani Tanganyika wadai uchunguzi fedha za ndani
30 August 2023, 10:03 am
TANGANYIKA
Madiwani wilayani Tanganyika wametaka kufanyika kwa ukaguzi wa ndani wa fedha za mapato ya ndani kutokana na fedha kuwepo lakini kushindwa kupelekwa kukamilisha miradi ya maendeleo iliyoanza kutekelezwa na wananchi.
Wakizungumza katika kikao cha robo ya nne ya mwaka wamesema wamelazimika kuazimia kutokana na miradi mingi kushindwa kutekelezwa licha ya pesa kupatikana na kupatikana kwa ripoti kutasaidia kujibu maswali ambayo wanajiuliza
Akijibu hoja hizo Kaimu Afisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Robert Magnus amesema kwa mujibu wa sheria miradi ambayo haijatekelezwa kwa mwaka husika wa fedha unapaswa kuombewa pesa upya kwa mwaka mwingine wa Fedha.
Katika hatua nyingine Kaimu Mkurugenzi wa Tanganyika Betuely Joseph Ruhega ameahidi kuwasilisha katika vikao vijavyo baada ya kufanyiwa kazi.