Mpanda FM
Elimu ya Afya ya Uzazi Inavyoweza Kusaidia Vijana Kuepuka Mimba za Utotoni
15 August 2023, 10:19 am
KASEKESE – TANGANYIKA
Kutokana na dhana iliyojengeka katika jamii kuwa ukimfundisha mtoto kuhusu Afya ya Uzazi unapelekea kujaribu mafunzo aliyopatiwa.
Mpanda radio fm imezungumza na baadhi ya wakazi wa kata ya Kasekese juu ya namna elimu ya afya ya uzazi inavyoweza kupambana na mimba za utotoni
Kwa upande wake Muuguzi Mkunga Wa Clinic ya Baba, Mama na Mtoto Agness Katapa amesema kuwa ni dhana isiyo na uhalisia huku akiwaasa vijana hasa jinsia ya kiume kujitokeza kwa wingi.
Kwa mujibu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kupitia kwa Naibu Waziri February 1, 2023 Amelieleza bunge kwamba kwa kipindi cha Mwaka 2021 na 2022 Wanafunzi 1554 wa Shule za Msingi na 7457 wa Sekondari Walipata ujauzito.