Mrindoko ‘Jiandaeni Kupokea Mwenge’
15 August 2023, 10:05 am
KATAVI
Mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewataka wananchi mkoani katavi kujiandaa na mapokezi ya mwenge wa uhuru ambao unatarajiwa kupokelewa August 24 katika shule ya msingi vikonge wilaya ya Tanganyika.
Ametoa taarifa hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, ambapo amesema mwenge wa uhuru utapokelewa kutoka katika mkoa wa Kigoma na Utakuwepo katika mkoa wa Katavi ukizunguka na kuzindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo, ambapo utazunguka katika halmashari zote na kuagwa tarehe 29 katika halmashauri ya mpimbwe na kukabidhiwa katika mkoa wa Rukwa.
Aidha mkuu wa mkoa wa Katavi amewataka wananchi kujitokeza katika maeneo yote ambayo mwege wa uhuru utakuwa ukipita kuzindua miradi mbalimbali ya kimaendeleo pamoja na maeneo ya mikesha, kuhakikisha wanasherekea kwa amani kama ilivyo tunu ya taifa ya amani.
Mwenge wa uhuru kwa mwaka 2023 unakimbizwa kwa kauli mbiu isemayo Tunza mazingira, Okoa vyanzo vya maji kwa Ustawi wa viumbe hai kwa uchumi wa Taifa
.