Kizungumkuti cha Nishati ya Mafuta
9 August 2023, 6:52 am
MPANDA
Baadhi ya Wakazi wa manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wakiwemo madereva wa vyombo vya moto wamaiomba serikali kuingilia kati hali ya upatikanaji wa mafuta Pamoja na bei ili kuleta unafuu wa maisha kwa mwananchi.
Maombi hayo wameyatoa wakati wakizungumza na mpanda radio fm juu ya bei mpya ya mafuta kwa mwezi huu wa nane pamoja na upatikanaji wake na kusema kuwa kuendelea kuongezeka kwa bei hizo kunachangia kupanda kwa gharama za usafiri jambo ambalo wamesema pia litachangia kupanda kwa bidhaa nyingine .
Wakizungumza juu ya hali halisi ya kipato cha mwananchi watumiaji wa vyombo vya moto Abiria wamesema kuwa kuendelea kuongezeka kwa bei za mafuta ni kikwazo kikubwa cha maendeleo kwa mwanchi wa kawaida .
Kila jumatano ya kwanza ya kila mwezi Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura) hutoa bei mpya za mafuta ya petrol dizel na mafuta ya taa ambapo kwa Manispaa ya Mpanda lita moja ya petroli imepanda kutoka sh 2800 ya mwezi uliopita mpaka sh 3357 kwa mwezi huu.