Mpanda FM

Marufuku kuacha moto ndani ya duka

30 June 2023, 10:34 am

KATAVI

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Katavi linaendelea na uchunguzi wa ajali ya moto iliyotokea katika duka moja soko kuu Mpanda huku likionya wanaoacha moto wakati wa kufunga maduka yao.

Kamishna msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Katavi Regina Kaombwe amekemea tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kuchoma ubani na udi na kuacha moto wakati wa kufunga maduka na kuondoka.

Katibu wa Soko Kuu la Mpanda Bwana Bernard Nswima ameiambia Mpanda Radio kuwa ili kuepusha ajali za moto kwenye baadhi ya maeneo sokoni hapo ni vyema wafanyabiashara wakazingatia maagizo yaliyowekwa likiwemo kutochoma udi na ubani pindi wanapomaliza shughuli zao.

Kauli ya Katibu wa Soko kuu la Mpanda imekuja kufuatia alfajiri ya Juni 25 kuzuka moto kwenye duka la mfanyabiashara aliyefahamika kwa jina moja la Mohamed na kuteketeza mali zilizokuwepo ambapo Mpanda Radio imezungumza na mlinzi wa soko hilo na kueleza namna alivokutambua tukio hilo.

#mpandaradiofm97.0

#jeshilazimamoto