Mpanda FM

Mpimbwe: Juhudi ziongezwe uhifadhi mazingira

30 June 2023, 10:07 am

MLELE

Jamii katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoani Katavi imeaswa kuongeza juhudi katika kuhifadhi mazingira.

Akifungua mkutano wa mwaka wa Jumuiya za watumia maji ngazi ya Jamii zilizo chini ya wakala wa usambazaji Maji na usafi na mazingira vjijini Ruwasa Halmashauri ya Mpimbwe mkuu wa Wilaya ya Mlele Majid Mwanga amesema jamii lazima iendelee na utaratibu wa Kupanda miti ili kuhifadhi vyanzo vya Maji.

Amesema kuwa ili huduma za upatikanaji wa Maji ziendelee lazima kwenda sambamba na zoezi la upandaji miti kwenye vyanzo vya maji kwa kuwa Maji ni Mhimu katika maisha ya kila siku ya mwanadamu katika shughuli mbalimbali.

Meneja wa Ruwasa Wilaya ya Mlele Charles Mengo amesema Ruwasa halmashauri ya Mpimbwe inaendelea kutekeleza miradi ya Maji kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma hizo kwa wananchi

Masanja Mongela Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikuba akichangia hoja katika kikao hicho ameishukuru Ruwasa kwa kufikisha Huduma ya Maji katika kijiji hicho na kuomba miundo mbinu iliyofungwa kwenye kijiji chake kuhakikisha inafanya kazi kwa ufanisi.

#mpandaradiofm97.0

#ruwasa

#mleledc