Sauti ya Katavi (Matukio)
7 June 2023, 5:40 pm
MPANDA.
Ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya usalama wa chakula diniani mkoa wa katavi ni miongoni mwa mikoa Tanzania inayozalisha mazao ya chakula kwa wingi licha ya kukabiliwa na changamoto ya utapia mlo na udumavu kwa watoto.
Kufuatia siku hii baadhi ya wazazi na walezi manispaa ya mpanda wameeleza kuwa licha ya uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula bado wanakabiliwa na ukosefu wa elimu ya kutosha inayohusiana na maswala ya lishe na chakula huku wazazi wenyewe wakitajwa kuwa chanzo cha utapia mlo na udumavu kwa watoto wao WILIAM LIWALI ANATULETEA UNDANI WA TAARIFA HII.
TANGANYIKA – KASINDE.
Baadhi ya wachimbaji wadogo wa Madini ya Copper Kijiji cha Kasinde wameuomba uongozi wa kijiji hicho kutatua mgogoro wa kimaslahi uliopo baina ya wachimbaji hao na uongozi wa Kijiji hicho.
Wakizungumza na Mwanahabari wetu Ben Gadau wachimbaji hao wamesema wameshtushwa baada ya kijiji kukabidhi machimbo kwa muwekezaji huku wakiongeza kwa kuuomba uongozi kuwalipa fidia ya kazi walizozifanya hapo awali.
KATAVI
Wananchi Mkoani Katavi wameombwa kuwa na Tahadhari na nyaya za umeme zinazokuwa chini wakati wa Zoezi la ukarabati wa Miundombinu ya Shirika la Umeme Tanzania TANESCO unaoendelea.
Henry Mwakifuna ametembelea maeneo ya Mpanda Hotel ambapo sehemu kubwa ya Nguzo za umeme zilizokuwa mbovu zimeondolewa na kuwekwa mpya na kisha kutuandalia taarifa ifuatayo .
MPANDA
Wanaume ambao wenza wao wana ujauzito manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wametakiwa Kwenda katika vituo vya kutolea huduma ya clinic kwa kuwasindikiza ili nao wapatiwe elimu hiyo inayotolewa .
Huku hayo yakiwa yanabainishwa inaelezwa kuwa sababu zinazochangia baadhi ya wanaume kutowasindikiza wenzi wao kwenye vituo vya kutolea huduma za clinic kwa wajawazito Mkoani hapa ni Pamoja na uelewa mdogo juu ya huduma hiyo na baadhi yao kuhofia majibu ya kipimo cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi HUYU HAPA VERONIKA MABWILE ANATUJUZA ZAIDI
DODOMA – KATAVI.
Baadhi ya wananchi mkoani katavi wametoa maoni yao juu ya kudhibiti ukwepaji kodi na biashara za magendo katika kuhimiza matumizi sahihi ya Tehama.
Maoni hayo yamekuja mara baada ya Waziri wa Fedha na mipango Dr Mwigulu Nchemba kusema bungeni hadi kufikia aprili 2023 wizara yake ilikuwa imechukua hatua mbalimbali zikiwemo kudhibiti matumizi ya serikali pamoja na mali za umma Tuungane na mwandishi wetu ANNASTAZIA FILIMBI kwa hundani wa taarifa hiyo.
MICHEZO
Mashindano ya UMITASHUMTA yamezinduliwa siku ya jana mkoani Tabora, NBC yatambulisha kombe jipya kwa msimu wa 2022/23 kimataifa Benzema na NG’olo Kante wajiunga na Al Itihad ya Saud Arabia.
Huyu hapa mwanamichezo Killian Samwel na taarifa hizo.