Sauti ya Katavi (Matukio)
26 May 2023, 10:57 am
MPANDA
Wadau wanaozalisha mazao yatokanayo na mifugo Mkoa wa Katavi, wametakiwa kufuata sheria, ikiwemo kuboresha usafi katika mabucha, na kuepuka matumizi ya magogo na vyuma vyenye kutu ili kulinda afya ya walaji.
Afisa Mfawidhi wa Bodi ya Nyama Kanda ya Magharibi, Joseph Kulwa wakati wakifanya ukaguzi, usajili na utambuzi wa mabucha katika mkoa ambapo amesema vitu walivyobaini ni wafanyabiashara wa nyama kuongeza mabucha bubu ambayo hayajasajiliwa ikiwa ni pamoja na kupima afya zao.
BETORD BENJAMIN AMEKUANDALIA SIMULIZI IFUATAYO
MPANDA
Wananchi wa Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kujenga desturi ya kufanya usafi wa mazingara kila siku katika maeneo yao sambamba na kutunza mazingira yanayowazunguka kwa lengo la kujikinga na magonjwa ya mulipuko yanayoweza kujitokeza katika jamii,Veronica mabwile ameandaa taaifa ifuatayo na kukufikishia hapa.
MPANDA
Wakazi wa Kitongoji cha Shankala Kijiji cha Sungamila Kata ya Kasokola Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameuomba uongozi wa eneo hilo kutafuta njia mbadala ya uhifadhi wa taka maji na taka kavu zinazotupwa karibu na makazi yao.
Wameyasema hayo wakati wakizungumza na Mwandishi wa Mpanda Radio Fm Lusy Dashud alipoenda kutembelea maeneo hayo na kuamua kupaza sauti zao juu ya kadhia hiyo wanayokumbana nayo.
KATAVI
Jeshi la polisi mkoani wa Katavi limewataka wafanya biashara wa mazao kujiepusha kutembea na fedha nyingi pindi wanapoenda kununua mazao.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi Ally makame Hamad akizungumza na waandishi wa Habari amesema kuwa kipindi cha mavuno hutoa mianya ya matukio mengi ya kihalifu na kuwataka wafanyabiashara kuomba ulinzi wanapokuwa na kiasi kikubwa cha fedha. JOHN BENJAMIN ANAKUJA NA UNDANI WA TAARIFA HIYO.
MICHEZO
Mchezo wa kirafiki kati ya Tigers FC na Malimao FC ulimalizika kwa sare 1-1, Simba sc watambulisha skauti mpya na kimataifa Manchester United kuminyana na Chelsea leo.
Mwanamichezo wetu Killian Samwel huyu hap ana taarifa hizo.