Mpanda FM

Sauti ya Katavi (Matukio)

23 May 2023, 10:38 am

KATAVI

Jeshi la Polisi Mkoani hapa Katavi kwa kushirikiana na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi wamewakamata watu wanne wakiwa na meno ya Tembo vipande 13 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 247.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Ali Hamad Makame   Amesema Katika tukio la kwanza watuhumiwa watatu Alex Ruben (45) Mkazi wa Kijiji cha Kapalamsenga Wilaya ya Tanganyika, Masele Kasema (36) Mkazi wa Kijiji cha Sitalike Wilaya ya Mpanda na Nkamba Ntemula (45) Mkazi wa Maji Moto Wilaya ya Mlele walikamatwa wakiwa na vipande saba vya meno yaTembo, kutoka ofisi ya kamanda wa polisi mkoani hapa Katavi JOHN BENJAMIN anakina cha taarifa hii.

MPANDA.

Wilaya ya Mpanda inaendelea kuboresha miundo mbinu mbalimbali ya kijamii ikiwemo barabara na afya huku zaidi ya shilingi bilioni tatu zilizotolewa na serikali zikielekezwa katika elimu pekee kwa halmashauri za Nsimbo na manispaa ya Mpanda.

Hayo yamezungumzwa na mkuu wa wilaya ya Mpanda Jamila Yusuph na kusema kuwa wilaya ya Mpanda inazidi kupokea miradi mbalimbali ikiwemo miradi ya maji, afya na barabara. WILLIAM LIWALI anaundani wa Habari hii.

KATAVI

Wananchi wa Mkoani hapa Katavi wameaswa kuondokana na kasumba ya kuthamini Bidhaa zinazotoka nje na kuthamini bidhaa zinazotengenezwa na Wazawa.

Mratibu wa Shirika la Viwango Tanzania TBS Manispaa ya Mpanda ambaye pia ni Afisa Afya Bwana Ambonisye Kyando ameiambia Mpanda Radio kuwa bidhaa za nyumbani zipo kwa Wingi na zinakidhi viwango.

Mwanahabari wetu Henry Mwakifuna ametembelea Viwanda vya Kusindika Mafuta, Mboga mboga na Matunda Manispaa ya Mpanda na kutuletea taarifa hii hapa.

NSIMBO

Wananchi wa kijiji cha Katisunga, kata ya machimboni halmashauri ya nsimbo manispaa ya mpanda Mkoani Katavi wameiomba mamlaka ya usimamizi na usambazaji wa Umeme Tanesco kutatua changamoto ya kukatikakatika kwa umeme inayowakabili kijijini hapo

Wameyasema hayo wakati wakizungumza na mwandishi wetu LUSY DASHUD alipofika kijijini hapo na kuongeza kuwa changamoto hiyo hupelekea kuungua kwa vifaa vyao.

MVOMERO

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Tumbeine Abdalah mwenye umri wa miaka 45 mkazi wa kijiji cha mkata wilaya ya mvomero mkoani morogoro ameuawa na tembo usiku wa kuamkia mei 20 mwaka huu baada ya kuchomwa na meno ya tembo mgongo na kutokea tumboni.

Tukio hilo linaelezwa si la kwanza kujitokeza katika maeneo hayo taarifa iliyoandaliwa na dawati la Habari inasomwa studioni na ANNA MILLANZI.

KAGERA

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoani Kagera Limefanikiwa kuthibiti moto usiku wa kuamkia leo mei 22, 2023 katika Soko kuu la Bukoba ambao umeteketeza maduka mawili.

Moto huo ulianza kuwaka majira ya saa tatu usiku wa mei 21 kwenye duka moja katika soko hilo ambapo jeshi la polisi pamoja jeshi la zimamoto wamefanikiwa kuthibiti moto pamoja na upotevu wa mali.

 BETORD BENJAMIN kutoka chumba cha habari anakuja na taarifa hiyo.

ARUSHA

Familia ya kijana alietambulika kwa jina la Evance anaeishi kata ya Akyeri wilayani Arumeru mkoani Arushai imetilia mashaka kifo cha kijana huyo aliefariki kwa kujinyonga huku mpenzi wake akiwa amefungwa kamba pembeni yake.

Baba mzazi wa kijana huyo anaeleza jinsi familia hiyo ilivotilia shaka kifo hicho na mzingira ambayo kijana huyo alikuwa amejinyonga na kuliomba jeshi la polisi kuchunguza kwa kina kifo cha kijana huyo. Taarifa iliyoandaliwa na dawati letu la Habari inasomwa hapa na KINYOGOTO FESTO.

MOROGORO

Jeshi la polisi Mkoani Morogoro linawashikiria watuhumiwa 23 kwa makosa mbalimbali ikiwemo utapeli kwa njia ya mitandao pamoja na Madawa ya Kulevya

Hayo yamebainishwa na kamanda  wa Polisi Mkoani humo Alex  Mkama wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya haabari na kuwataka wananchi Mkoani humo  kushirikiana na jeshi hilo kutoa taarifa ili kuwabaini waharifu .Veronica Mabwile ametusomea taarifa hiyo kutoka chumba cha habari 

MICHEZO

Mtoto wa nyumbani hapa Katavi na mwanamasumbwi Ngumi jiwe ashinda kwa TKO pambano lake alilocheza Dubai Weekend hii Pia Mafunzo ya waamuzi yahitimishwa mkoani hapa Zaidi ya waamuzi 80 wamepatiwa mafunzo hayo Na Kimataifa NBA kuendelea leo hii.

Mwanamichezo wetu Killian Samwel anaundani Zaidi wa taarifa hizo.