Barabara ya Mpanda – Karema Mbioni Kuanza Ujenzi
12 May 2023, 8:15 am
TANGANYIKA
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi anae shughulikia Sekta ya Ujenzi Ludovick Nduhye amefanya ziara ya kutembelea barabara ya kutoka Mpanda kwenda Bandari ya Karema ambayo inatarajiwa kuanza kujengwa hivi karibuni mwaka huu kwa kiwango cha lami .
Akizungumza Nduhye amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kuangalia barabara inayotarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami mahali inapo anzia na inapoishia .
Amebainisha kuwa lengo la Serikali ya awamu ya sita ni kuboresha miundo mbinu ya mawasiliano ya barabara katika kuhakikisha inakuza uchumi wa nchi na kwa watanzania kwa ujula ambapo ujenzi wa barabara ni muhimu kwa Nchi ya Tanzania na Kongo kwa kusafirisha mizigo kupitia bandari ya Karema.
Meneja wa Tanroads Mkoa wa Katavi Mwandisi Martin Mwakabende ameeleza kuwa taratibu za kuwapata wakandarasi watakao tengeneza barabara hiyo tayari umeisha anza kwa kutangaza tenda ya kandarasi hiyo .
Amefafanua kuwa zabuni za kuwapata wakandasi wa barabara hiyo utafanyika tarehe 30 ya mwezi huu wa tano ambapo itakuwa siku ya kufunga na kuruhusu uchambuzi wa tenda zitakazokuwa zimeombwa na makampuni ya ujenzi wa barabara na ujenzi huo utachukua muda wa miezi 24.