Mpanda FM

Nsimbo Walia na Utapiamlo

12 May 2023, 5:50 am

MPANDA.

Halmashauri ya Nsimbo mkoani Katavi inakabiliwa na changamoto ya utapia mlo licha ya kuzalisha mazao mengi ya chakula.

Hayo yamesemwa na kaimu mganga mkuu hospitali ya halmashauri ya wilaya ya Nsimbo daktari Wambura Waryoba katika mkutano wa taarifa kwa kamati ya lishe ya wilaya juu ya utekelezaji wa afua za lishe kwa robo ya tatu ya mwaka 2022/2023 na kusema kuwa hali ya utapia mlo kwa halmashauri hiyo ni asilimia 33.7 kwa mwaka wa fedha uliopita na asilimia 32.2 kwa mwaka huu wa fedha.

Kwa upande wake afisa lishe wa halmashauri ya wilaya ya Nsimbo Nickson Yohanes amewataka wananchi wa halmashauri hiyo kuzingatia makundi Matano ya vyakula katika mlo ili kuondokana na changamoto ya utapia mlo huku akisisitiza matumizi ya chumvi zenye madini joto.

Rehema Mbuya mratibu wa mama baba na mtoto halmashauri ya Nsimbo amewataka wakina mama kuzingatia lishe ili kuimalisha afya ya mtoto awapo tumboni huku akiwahimiza kutumia vidonge vya kuongeza damu miezi mitatu kabla ya ujauzito.

#mpandaradiofm97.0

#wizarayaafya