Mabaki ya Mazao na Utunzaji wa Mazingira
16 April 2023, 3:17 pm
KATAVI
Ili kuinua uchumi na kusaidia kulinda mazingira Wananchi mkoani Katavi wameaswa kutumia majiko Banifu katika shughuli zao.
Mtaalamu wa Masuala ya Mazingira Manispaa ya Mpanda Bwana Prosper Mwesiga amesema kuwa matumizi ya Majiko banifu yanasaidia kwa kiwango kikubwa upunguzaji wa uchafuzi wa mazingira.
Amesema kuwa matumizi ya mabaki ya mazao kama karanga, makapi ya mpunga na maranda ya Mbao yanaasaidia kupunguza gharama za matumizi nakuokoa mazingira.
Kwa upande wa mtengenezaji wa majiko Banifu Stanley Kitika amesema kuwa majiko hayo ni nafuu na yanasaidia kuokoa gharama na yanapatikana kwa muujibu wa mahitaji ya mteja.
Baadhi ya watumiaji wa majiko hayo wamesema kuwa ni gharama nafuu katika upatikanaji wa majiko na Rasilimali makapi yatumikayo kama nishati katika kupikia Na kuwataka wakazi kutumia teknolojia hiyoambayo ni rafiki kwa mazingira ili kuendana na maagizo ya serikali .