Mpanda FM
Ajira kwa Watoto Bado Changamoto Katavi
22 February 2023, 6:42 pm
KATAVI
Wananchi Halmashauri ya manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wamelaani wazazi wanaoruhusu watoto wadogo kufanya biashara muda ambao walitakiwa wawe shule.
Wakizungumza na kituo hiki wananchi hao wamesema kuwa vitendo hivyo vinaathiri saikolojia za watoto na kuwapotezea malengo yao ya baadae.
Aidha watoto wameainisha sababu zinazowapelekea kujikita kwenye shughuli za utafutaji kuwa ni kukosa mahitaji yao kutoka kwa wazazi hivyo inawalazimu kufanya kazi ili kukidhi baadhi ya mahitaji yao.
Judithi ni Ispector kutoka dawati la jinsia mkoani Katavi, amewataka wananchi kuripoti wazazi wasio watimizia watoto wao mahitaji ya msingi ili serikali iwashurutishe na kuwawajibisha katika suala la malezi.