Mpanda FM

Mtapenda Yaendeleza Kampeni ya Upandaji Miti

22 February 2023, 6:18 pm

NSIMBO

Katika kuunga mkono Kampeni ya serikali ya upandaji wa miti kata ya Mtapenda Halmashauri Ya Nsimbo Mkoani Katavi imeanza zoezi la upandaji wa miti katika vijiji vyake kwa lengo la kuendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Wakizungumza na Mpanda Radio fm wananchi Walioshiriki zoezi wamesema kuwa njia pekee ya utunzaji wa mazingira ni kujikita katika kupandaji wa miti huku wakiitaka serikali kuwachukulia hatua wafugaji wanaolisha mifugo katika maeneo yaliyopandwa miti.

Kwaupande wake Diwani wa kata hiyo Elieza Fyula amesema kata hiyo imepanga kupanda miche elfu ishirini ya miti ambapo kila Kijiji kitapanda miche elfu tano na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kutekeleza zoezi hilo ambalo amesema ni endelevu

Kwaupande wa viongozi walioshiriki tukio hilo wamesema miti hiyo itasaidia kuongeza hali ya uzalishaji sambamba na kuongeza tija kwa wakazi wa kata hiyo

Upandaji wa miti ya kutosha katika maeneo yanayomzunguka mwanadamu husaidia upatikaji wa mvua yakutosha ikiwa ni pamoja kuongeza hali ya hewa safi kwa viumbe hai wengine.