Elimu Itolewe Juu ya Ugonjwa wa KifuaKikuu
16 February 2023, 6:06 am
MPANDA
Serikali Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi imetakiwa kuongeza juhudi za utoaji wa elimu ya ugonjwa wa Kifua Kikuu ili kuwapatia wananchi uelewa juu ya ugonjwa huo
Hayo yamebainishwa na wananchi wa Manispaa ya Mpanda wakati wakizungumza na Mpanda Radio fm kuhusu uelewa namna ugonjwa unavyoambukizwa ambapo Baadhi wamesema kuwa hawana uelewa wowote juu ya ugonjwa na namna unavyoenezwa.
Kwa upande wake Mratibu wa ugonjwa wa kifua kikuu na ukoma Manispaa ya Mpanda Daktari Bruno Cronwel Handilo amesema hali ya maambukizi ya ugonjwa huo inaonekana kuongezeka hivyo na kuitaka jamii kuendelea kuchukua tahadhari na kufuata taratibu zote zinazotolewa na wataalamu wa afya namna ya kuepukana na kifua Kikuu.
Kwa kipindi cha mwaka 2022 wananchi zaidi ya 400 waligunduliwa kuwa na ugonjwa huo ambapo waathirika wa ugonjwa wa kifua kikuu kwa kiasi kikubwa wakionekana ni vijana na watoto