Mpanda FM

Katavi Bila Malaria Inawezekana

20 January 2023, 3:18 am

MPANDA

Ili kujikinga na ugonjwa wa Malaria wananchi manispaa ya mpanda mkoani katavi wameshauriwa kutokomeza maeneo yote ambayo yanaweza kuwa ni chanzo cha mazalia ya mbu sambamba na kutumia chandarua wakati wa kulala.

Ushauri huo umetolewa na mganga mkuu manispaa ya mpanda Paul Swakala wakati akizungumuza na Mpanda Redio fm nakusema kuwa wananchi wanatakiwa kufyeka majani na kufukia madibwi yote ya maji yanayozunguka makazi yao .

Kwa upande wao wananchi wamesema wataendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa malaria ikiwa ni pamoja na kufyeka majani na kufukia madibwi yote ya maji yanayo zunguka makazi yao na kulala kwenye chandalua kila siku ili kujikinga na ugojwa huo.

uwepo wa vichaka na madimbwi ya maji katika makazi ya watu imetajwa kuwa chanzo kikubwa kinachozalisha mbu jike aina ya anoferesi hali inayopelekea kuzidi kuenea kwa ugonjwa huo.