Maambukizi mapya ya VVU Manispaa ya Mpanda yashuka mbaka 3.5%
1 December 2022, 10:38 pm
MPANDA
Katika kuadhimisha siku ya ukimwi duniani Manispaa ya mpanda imefanikiwa kupunguza maambukizi mapya ya virusi na kufikia asilimia 3.5.
Akizungumza na mpanda radio fm mganga mkuu manispaa ya mpanda dk paul swankala amesema takwimu ya 3.5 inamaanisha kila wagonjwa 100 watu watatu hadi wanne wameathirika na kuwataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kujikinga na maambukizi mapya.
Katika hatua nyingine Swankala ametoa wito kwa kwa wanaokutwa maambukizi ya virusi vya ukimwi kutumia bila kuacha dawa za kufubaza viruzi vya ukimwi ili kupunguza maambukizi manispaa na mkoa kwa ujumla.
Mkoa wa Katavi unaungana na mikoa mingine Nchini kuadhimisha siku ya UKIMWI Duniani yanayofanyika katika uwanja wa shule ya msingi kasekese, mkuu wa mkoa wa katavi mwanamvua mrindoko Anakuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo na kauli mbiu inasema, Imarisha Usawa.