Mpanda FM

Wachimbaji Wadogo wa Madini Waomba Uongozi wa Kijiji Kutatua Mgogoro Kati Yao na Wananchi

21 October 2022, 11:36 am

MPANDA

Wachimbaji wadogowadogo wa madini katika kitongoji cha Kagera kijiji cha dirifu kata ya Magamba wameuomba uongozi wa kijiji hicho kutatua mgororo uliopo baina ya kikundi cha Kagera  Group na wananchi.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara wa kijiji hicho wamesema  mgogoro huo unatokana na kikundi cha Kagera Group kujimilikisha mlima kwa shughuli za uchimbaji wa madini bila ridhaa ya wananchi kwa kijiji hicho.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Bi Marieta Mlozi Afisa Maendeleo Manispaa ya Mpanda amesema wanakijiji pamoja na kikundi hicho wanapaswa kumaliza tofauti zao kwa kupitia upya nyaraka ikiwemo leseni inayo waruhusu wao kumiliki mlima huo na kama kuna makosa hatua stahiki zifuatwe.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Magamba Fortunatus Michael Chiwanga amesema kikundi cha Kagera Group hakina mamlaka ya kumiliki mlima huo kwa ajili ya shughuli zao za uchimbaji na badala yake amewaruhusu wanakijiji hao kuendelea na uchimbaji wa madini katika eneo hilo.

Inatajwa kuwa Mgororo baina ya wananchi wa kijiji hicho na kikundi cha Kagera Group umeanza tangu mwaka 2016 baada ya uongozi wa awali kubadilika na umedumu kwa takribani miaka miaka sita hadi kufikia october 20,2022.