Tanesco Wapewa Wiki Tatu Kufikisha Umeme Hospital Mpya ya Mkoa
20 October 2022, 5:24 am
MPANDA
Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amewataka Shirika la umeme mkoa wa Katavi ndani ya wiki tatu kuhakikisha umeme unafika katika hospitali mpya ya mkoa wa Katavi
Akitoa maagizo wakati akijibu taarifa ya mganga mfawidhi wa hospitali teule ya mkoa, mkuu wa mkoa wa Katavi amesema wanapaswa kutekeleza agizo hilo ili kuwapunguzia wananchi adha ya kupata rufaa ya Kwenda hospital kubwa kutokana na vifaa vilivyowekwa nan kushindwa kufanya kazi kwa sababu ya kukosa umeme unaohitajika.
Awali akitoa taarifa kwa mkuu wa mkoa kuhusiana na maendeleo ya ujenzi wa hospital mpya ya mkoa Dk Seraphine Patrice amesema baaadhi ya mnajengo yameshakamilika na mitambo ishawekwa huku changamoto ni upatikanaji wa umeme.
Kwa mujibu wa maelekezo ya serikali yaliyotolewa na serikali chini ya wizara ya afya mwezi wa 9 mwaka huu hospital hiyo inapaswa kuanza kufanya kazi tarehe 14/11/2022.