Wazazi Wapongeza Matibabu ya Mguu Fundo
14 October 2022, 5:25 am
Wazazi ambao wana watoto wenye ugonjwa wa Mguu kifundo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wamepongeza uwepo wa matibabu ya mguu kifundo katika hospitali ya rufaa Mkoani hapa.
Wakizungumza na Mpanda radio fm wazazi wamesema wengi waligundua ugonjwa walipozaliwa na kufanya uamuzi wa kuwapeleka hospitali huku wakieleza kuwa Huduma zinazotolewa katika hospitali iyo ni nzuri.
INSERT…. WAZAZI
Kwa upande wake Mtoa huduma ya afya kuhusiana na mguu kifundo daktari Wilium Thomas amesema Mguu kifundo ni aina ya ulemavu ambao mtoto anazaliwa nao watoto wengi hupata tatizo hilo na hakuna sababu maalumu za ugonjwa na unagundulika mara baada mama mjamzito kujifungua.
INSERT ….DOKTA THOMAS
Aidha Dokta wilium amewataka wazazi ambao wanajifungua watoto ambao wanaugonjwa huo kuwafikisha hospitali ili waweze kupatiwa matibabu ambayo yanatolewa bure.