Mpanda FM

Vijana Mkoani Katavi Wahitaji Elimu Zaidi juu ya Afya ya Akili

11 October 2022, 11:07 am

KATAVI

Katika Kuadhimisha Kongamano la Kwanza la Kitaifa la Afya ya Akili, baadhi ya vijana Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameonyesha kutokua na uelewa juu ya tatizo la  Afya ya Akili .

Wameyasema ayo wakati wakizungumza na Kituo hiki huku wengiwao wakionyesha uhitaji wakufahamu zaidi juu ya tatizo hilo.

Daktari Kitengo cha Magonjwa ya Ndani Hiberi Msigwa kutoka Hospital ya Rufaa Mkoani hapa  amesema kuwa zipo sababu nyingi zinazopelekea mtu kupata tatizo hilo ikiwemo kurithi,mtindo wa maisha na matumizi makubwa ya vilevi .

Nae Emmanuel Tinda Afisa Uhusiano Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha wanatoa huduma zilizo bora kwa wananchi wanaokumbana na tatizo hilo.

Kila ifikapo tarehe 10 october Dunia huadhimisha siku ya Afya ya Akili ikiwa maalum kwa kutoa elimu ya masuala ya afya ya akili , uhasmasishaji na utetezi dhidi ya unyanyapaa wa kijamii pamoja na athari zake.