Watembea kwa Miguu Walia na Waendesha Vyombo vya Moto
16 September 2022, 4:07 am
MPANDA
Baadhi ya watembea kwa miguu katika manispaa ya mpanda mkoani katavi wamewalalamikia madereva wa vyombo vya moto kutozingatia sheria na alama za usalama barabarani pindi wanapoendesha.
Wakizungumza na mpanda redio fm wananchi hao wameeleza kuwa wanakutana na changamoto ya kunyimwa uhuru wa kutumia barabara kwa kuhofia kusababishiwa ajali na madereva kwa kutozingatia alama za usalama barabarani.
.
Kwa upande wake askari wa usalama barabarani kutoka ofisi ya RTO John Shindika amesema kuwa idadi kubwa ya madereva ambao hawazingatii alama za usalama barabarani ni wale ambao hawajasoma udereva na kusema kuwa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani hakitasita kumchukulia hatua za kisheria kwa yeyote atakae vunja sheria za usalama barabarani.
.
Hivi Karibuni kumeripotiwa Ajali nyingi ambazo zimetokana na baadhi ya madereva kutozingatia sheria na alama za usalama barabarani .