Mpanda FM

Bil.40 za Mradi Kunufaisha Huduma za Malaria Mkoani Katavi

15 September 2022, 9:55 pm

KATAVI

Mkoa wa Katavi umepokea mradi wa miaka mitano utakao gharimu Bilioni 40 unaosimamiwa na serikali  ya Marekani chini ya taasisi ya afya ya Ifakara  utakoshirikiana  na Mkoa kusimamia huduma za Malaria .

Akizungumza wakati wa kutambulisha mradi huo mkurungezi wa mradi kutoka taasisi ya afya Ifakara Dokta Dustani  Bishanga amesema mradi huu unalenga kuboresha huduma za malaria kwa kutoa elimu kwa wananchi, kuwaongezea elimu watumishi wa afya pia kuboresha mifumo ya  afya.

.

Katibu tawala wa mkoa wa katavi Hassan Abbas Rungwa akizungumza baada ya kupokea mradi amesema mradi huo umekuja kwa wakati sahihi kutokana na hali ya malaria mkoani hapa na kuahidi kutoa ushirikianao katika utendaji na usimamizi .

.

Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa inayoongoza  katika takwimu  za malaria nchini hivyo utekelezaji wa mradi wa kuzuia malaria unalenga kupunguza hali ya maambukizi  malaria nchini. Mostbet Online Casino in India 2024