Wananchi Watakiwa Kuwa Wavumilivu Maboresho ya Barabara
8 September 2022, 6:49 pm
IVUNGWE- MPANDA
Siku chache tangu barabara ya ivungwe kuanza kurekebishwa kwa ahadi ya mbunge Sebastiani Kapufi wananchi wametakiwa kuwa wavumilivu wakisubiri kumalizika kwa mradi huo kutokana na changamoto ya kuharibika kwa mtambo wa kutengeneza barabara hiyo.
Akizungumza kwa njia ya simu Mwenyekiti wa kijiji cha Kasokola Carlos Joackim Mwalufa amesema utekelezaji wa barabara hiyo ulishaanza katika baadhi ya maeneo ya Ivungwe .
.
Awali Wananchi wakizungumza na Mpanda radio fm walisema kuwa kwa kipindi kirefu wamekuwa wakichelewa kupata huduma ya afya kwa haraka kutokana na ubovu wa barabara kufika zahanati kupata huduma ya afya na kuomba serikali kuwasadia kuboresha barabara.
.
Kuboresha kwa barabara kutoka ivungwe -kasokola umeanza kutekelezwa baada ya ziara ya mbunge wa jimbo la Mpanda mjini Sebastian Kapufi Ivungwe kusikiliza kero za wananchi ambapo wamekuwa wakitumia barabara iliyoharibika kufuata huduma ya afya takribani kilomita kumi katika kijiji cha kasokola.