Mpanda FM

Wananchi Mkoa wa Katavi waachana na tahadhari za UVIKO 19

6 September 2022, 10:23 am

KATAVI

Baadhi ya Wananchi mkoani Katavi wameonekana kuacha kuzingatia tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Uviko 19 tofauti na ilivyokua hapo awali.

Mpanda radio imepita katika maeneo mbalimbali mkoani hapa na kubaini kuwa hakuna tahadhari yeyote inayochukuliwa ya kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kuvaa barakoa,kukaa kwa kuzingatia umbali wa mtu mmoja na mwingine hasa katika maeneo yenye mikusanyiko.

Hata hivyo maeneo ya biashara na ofisi mbalimbali bado zimeweka ndoo za maji safi na vitaka mikono licha ya kutotumiwa na watu wanaofika katika maeneo yao.

Wakizungumza na kituo hiki  wananchi hao wamesema kuwa hakuna mkazo dhidi ya ugonjwa huo hali iliyopelekea kuacha kujikinga na ugonjwa huo.

.

Hivi karibuni Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani alitoa agizo kwa wizara ya Afya kuangalia mwenendo wa janga la  UVIKO 19 nchini.

.

Raisi Samia amewataka watanzania kuendelea kuchukua tahadhari  ya  UVIKO 19 kwa kuwa janga hilo bado lipo.