Mpanda FM

USIRI KWA WANAUME UNAVYOCHANGIA CHANGAMOTO YA AFYA YA AKILI

8 June 2022, 4:03 pm

Wananchi mkoani katavi wametoa maoni yao juu ya kwanini usiri kwa wanaume unapelekea kusumbuliwa na changamoto ya afya ya akili.

Wamyasema hayo wakati wakizungumza na Mpanda Radio Fm na kusema kuwa hiyo ni kwasababu wanaume wengi si wazungumzaji wa vitu vinavyowasumbua kama ilivyo kwa wanawake hali inayopelekea wao kuathiriwa zaidi ya wanawake.

Kwa upande wake Mtaalamu wa Magonjwa ya Akili Emmanuel Kipande amesema kuwa ni muhimu vijana wakafuatilia maswala ya Afya ya akili ili kuweza kufanya shughuli za maendeleo katika jamii inayomzunguka huku akibainisha kuwa  si rahisi kwa mtu mwenye changamoto ya afya ya akili kuweza kujitambua kuwa anachangamoto hiyo.

Kwa mujibu wa daktari bingwa wa magonjwa ya akili kutoka hospitali ya muhimbili, Dkt. Praxeria Swai wanaume wanaweza kujiua mara tatu zaidi ya wanawake ambao huwa wanaishi na mawazo hayo.