TAKUKURU: WANANCHI TUSHIRIKIANE KUTOMEZA RUSHWA
25 May 2022, 4:23 pm
Jamii mkoani katavi imeaswa kushirikiana na tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa takukuku katika kutokomeza vitendo vyote vya rushwa mkoani hapa.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Takukuru Mkoani katavi Festo Mdede wakati akitoa taarifa ya utendaji kazi wa ofisi ya takukuru kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia January hadi March Mwaka huu.
Aidha mdede ameeleza kuwa kuna wimbi la matapeli wanaojitambulisha kam mafisa wa takukuru na kuwa pigia watu simu kwa ajili ya kujipatia fedha hivyo ameomba wananchi kutoa taarifa kwa ofisi ya takukuru wanapokutana na watu wa namna hiyo.
Katika hatua nyingine mkuu huyo amesema wamefuatilia utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule za sekondari na vituo shikizi na kubaini ubadhirifu wa miradi hiyo hivyo kuwataka waliotengeneza samani chini ya kiango warudie kwa gharama zao binasi na wakihakikisha mafundi waliomaliza kazi wanalipwa.