MAZIWA NA UTOKOMEZAJI WA UDUMAVU KATAVI
23 May 2022, 2:20 pm
Wazazi na walezi mkoani katavi wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika maadhimisho ya siku ya maziwa yatakayofanyika kuanzia tarehe 27 had tarehe moja mwezi wa sita mwaka huu ili kujifunza umuhim wa maziwa katika mwili wa mwanaadam na hatimae kuondokana na tatizo la udumavu .
Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa mkoa wa katavi Mwanamvua Hoza Mrindoko amewasisistiza wafanyabishara, wawekezaji na wafugaji kujitkeza kwa wingi kupata elimu ya namna ya kutumia teknolojia bora ya upatikanaji wa maziwa na ufugaji.
Kwa upande wake Afisa mifugo Mkoani hapa Zidiel Muhando amesema kuwa mkoa wa katavi unazalisha lita milioni 23 za maziwa kwa mwaka huku akibainisha kuwa kiwanda cha kusindika maziwa kimekamilika hivyo kukamilika kwake kutaongeza unywaji wa maziwa kwa wananchi na hatimae kuboresha afya .
Maadhimisha ya siku ya maziwa yanatarajia kufanyika kitaifa mkoani hapa yakiwa na kaulimbiu isemayo ‘kunywa maziwa yaliyosindikwa Tanzania kwa lishe bora na salam’.