MGANGA WA KIENYEJI MBARONI KWA ULAWITI
23 May 2022, 1:32 pm
Jeshi la polisi mkoani katavi limefanikiwa kumkamata mganga wa kienyeji akili abakuki almaarufu kama jimmy mwenye umri wa miaka 38 mkazi wa majengo kwa tuhuma za kulawiti watoto wenye umri kati ya miaka 6 hadi 12 alipokuwa akiwapatia matibabu ya tiba asilia.
Akizungumza na waandishi wa habari kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Sylvester Ibrahim amesema mganga huyo amekamatwa mei 8 mwaka huuu baada ya mama mmoja kusikia kutoka kwa watoto wake wakihadithiana namna mganga huyo alivyo wafanyia vitendo hivyo.
Mpanda radio fm imekutana na mmoja wa wazazi ambae mtoto wake wa tatu wamefanyiwa vitendo hivyo na kueleza kuwa mganga huyo alikuwa akihimiza kulala na watoto hao pamoja kwa madai ya kuwafanyia tiba za usiku licha ya yeye kutofaham kilichokuwa kikiendelea.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kata ya makanyagio athumani lubwe amekiri kumpokea mganga huyo mwezi wa sita mwaka 2021 akiwa anaitaji kupewa makazi katika kata yake.
Afisa mahusiano hospital ya rufaa mkoani hapa Emanuel tinda amethibitisha kupokea watoto saba ambapo kati yao wakike wakiwa ni wa 3 na wakiume 4 huku akisema kuwa kwa watoto wa kiume imekuwa vigumu kutambulika kuafanyia vitendo hivyo kwa kuwa ni mda sasa tangu wafanyiwe viytendo vivyo.
Hata hivyo jeshi la polisi mkoani hapa limetoa rai kwa wananchi kuendelea kuwa fichua watu wenye mienendo ama viashiria vya kihalifu kwani matokeo vya vitendo hivyo hukwamisha maendeleo ya jamiii nzima.