DC TANGANYIKA UMEME KAREMA KABLA YA MAY 20
23 May 2022, 1:03 pm
KATAVI.
Mkuu wa wilaya ya tanganyika onesmo buswelu amelitaka shirika la umeme mkoa wa katavi kuunganisha umeme katika bandari ya karema kabla ya may 20 mwaka huu kwakuwa mradi huo upo katika hatua za mwisho kukamilika.
Buswelu ametoa angizo hilo katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya mradi Ambapo amebaini kubaini changamoto ya tanesco kusuasua kuunganisha umeme katika bandari hiyo.
Awali mshauri wa mradi huo mhandisi eliasante edward amesema umefikia asilimia 91 na kwamba upo hatua za ukamilishaji wa miundombinu ya umeme pamoja na maji katika bandari hiyo.
Katika hatua nyingine Mpanda radio fm imezungumza na wananchi wa karema Ambapo wamepongeza jitihada za serikali kufanikisha mradi huo, huku kilio chao kwa rais Rais Samia suluhu Hassan ni barabara ya karema –mpanda kujengawa kwa kiwango cha lami ili kufungua fursa za bandari.
Mpaka sasa mradi ambao unaotegemewa kuwa kitovu cha uchumi kwa mkoa wa katavi na nchi za jirani ikiwemo Kongo umekamilika kwa 91 huku ukiwa unategemewa kuanza kufanya majaribio ya mitambo.