Elimu ya Uraia Itolewe
19 November 2021, 12:33 pm
Wananchi wa wilaya ya mpanda mkoani katavi wameiomba serikali kupitia idara ya uhamiaji kutoa elimu ya uraia ili kuwajengea wananchi uelewa katika masuala ya uraia.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mpanda redio baadhi ya wananchi wamesema hawana elimu ya kutosha inayomuwezesha kutambua nani ni raia wa Tanzania na nani si raia wa Tanzania hivyo wameiomba serikali kutoa elimu zaidi.
Kwa upande wake Inspekta wa uhamiaji wilaya ya mpanda Victor Saulo ameeleza kuwa ili mtu aweze kutambulika kama raia wa Tanzania sio tu kwa kuzaliwa ndani ya ardhi ya Tanzania bali vipo vigezo mbalimbali ambavyo vinamtambuliasha mtu kuwa ni raia halali.
Mkoa wa katavi ni moja ya mikoa iliyo mipakani ambapo inakabiliwa na wimbi kubwa la kuingia kwa wahamiaji haramu kinyume cha sheria na kuweka makazi.