Mufti Mkuu Tanzania: Bakwata tafuteni hati
13 October 2021, 8:58 am
- OKTOBA 6, 2021
KATAVI
Mufti na Shekh Mkuu wa Tanzania Abubakar bin Zuberi amewataka makatibu wa misikiti yote Mkoani katavi kuhakikisha wanapata hati miliki za viwanja vyote vinavyomilikiwa na baraza la waislam Tanzania BAKWATA.
Shekh mkuu wa Tanzania ameyasema hayo alipotembelea shamba la mikorosho linalomilikiwa na baraza hilo mkoani hapa na kueleza kuwa ili kuondokana na migogoro ya ardhi ni vyema ardhi hizo zikapatiwa hati miliki.
Akitoa taarifa ya shamba hilo katibu wa msikiti wa madina Khalid Chibila amesema kuwa shamba hilo la mkororosho linathamani ya shilingi Milioni Moja na Laki Tatu huku akibainisha kuwa mpaka ifikapo 2023 wanatarajia kuvuna korosho katika shamba hilo.
Muft na Shekh mkuu wa Tanzania yupo mkoani katavi kwa ziara ya siku mbili ya ukaguzi wa miradi mbalimbli ya baraza kuu la waislam Tanzania.