Jamii FM

Mjumbe wa H/kuu CCM asisitiza viongozi kuonesha uongozi kwa vitendo

13 December 2024, 12:39 pm

Hii ni baada ya matokeo ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika November 27,2024 ambapo viongozi wamechaguliwa na tayari wameanza kuwatumikiwa wananchi.

Na Musa Mtepa

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mtwara, Bi. Zuhura Farid, amewataka viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi wa serikali za mitaa kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi, badala ya kuendelea na makundi yaliyojitokeza wakati wa uchaguzi.

Ametoa wito huo akiwa katika hafla ya kumpongeza Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyengedi kwa kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo kama mwanamke pekee na wa kwanza kushika wadhifa huo.

Katika hotuba yake, Bi. Zuhura amesisitiza umuhimu wa viongozi wa serikali za mitaa kushirikiana na viongozi wa chama na kuachana na migawanyiko ya kisiasa.

Sauti ya Zuhura Farid Mjumbe wa halmashauri kuu CCM mkoa wa Mtwara.

Aidha, Mwanahamisi Abdala Magimbi, Mjumbe wa Viti Maalum CCM kutoka Kata ya Mkunwa, amesisitiza kuwa wananchi wana imani kubwa na viongozi waliochaguliwa, hivyo ni jukumu la viongozi hao kuonesha kwa vitendo yale yaliyoahidiwa wakati wa kampeni.

Pia amempongeza Mwenyekiti wa Kijiji cha Nyengedi kwa kuchaguliwa kwake na kumtaka kuwa tayari kukabiliana na changamoto za wananchi.

Sauti ya 1 Mwanahamisi Magimbi mjumbe viti maalum ccm kata ya Mkunwa