Shirika la ADEA laendelea na mafunzo kwa mafundi seremala Mtwara
26 November 2024, 16:05 pm
Na Mwanahamisi Chikambu
Katika muendelezo wa mafunzo ya sanaa katika kituo cha makumbusho cha MAKUYA kilichopo chini ya shirika la ADEA mtaa wa Sinani, Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya ADEA, Said Chilumba, amewataka vijana ambao ni mafundi seremala kuchangamkia fursa ya mafunzo yanayotolewa na shirika linalojihusisha na sanaa na utamaduni mkoani Mtwara, la ADEA, ikiwa na lengo la kuboresha kazi wanazozifanya kila siku.
Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo leo, Novemba 26, 2024, Chilumba amewataka mafundi seremala kuwa wabunifu katika kazi wanazozifanya ili bidhaa hizo ziweze kuongeza thamani na kutambulisha utamaduni wa wanamtwara.
Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Sharifu Mapila, ameelezea namna mafunzo hayo yatakavyowawezesha mafundi seremala kutengeneza samani tofauti na mafundi wengine,na kuweza kuuza bidhaa hizo na kusadia kuboresha maisha yao ya kila siku na kujitangaza kimataifa.
Sauti ya Sharifu Mapila
Kwa upande wao, washiriki wa mafunzo mafundi seremala wamesema kwamba mafunzo hayo yatawaongezea ujuzi na ubunifu, na kuweza kutengeneza samani bora na za kipekee zitakazotofautisha na kazi za mafundi wengine ambao hawajapata mafunzo hayo.