Jamii FM

Kaimu Shekhe Mkuu wa Mtwara Ahamasisha kujiandikisha katika orodha ya wapiga kura

16 October 2024, 14:40 pm

Kaimu shekhe mkuu wa mkoa wa Mtwara ,Shekhe Jamaldin Chamwi akizungumza na waandishi wa habari juu ya umuhimu wa uchaguzi wa serikali za mitaa(Picha na Grace Hamisi)

Uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika November 27,2024 uendane na sambamba na kutunza tunu ya amani iliyopo nchini “kwani Tanzania inajukana kama kisiwa cha amani hivyo,jamii haiana budi kutunza tunu hiyo”Shekhe Jamaldin.

Na Grace Hamisi

Kaimu Shekhe mkuu wa mkoa wa Mtwara, Jamaldin Salimu Chamwi, ametoa wito kwa jamii ya Wanamtwara kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.

Akizungumza na waandishi wa habari, Shekhe Jamaldin amesisitiza umuhimu wa kutumia muda uliobaki ili kupata kibali cha kupiga kura.

Sauti ya 1 Shekhe Jamaldin Salimu Chamwi ,kaimu shekhe mkuu wa mkoa wa Mtwara

Pia, amehimiza Watanzania kushirikiana katika kutunza amani na usalama wa nchi, akiwataka kuacha kujihusisha na vikundi vinavyoweza kuleta machafuko.

Sauti ya 1 Shekhe Jamaldin Salimu Chamwi ,kaimu shekhe mkuu wa mkoa wa Mtwara