Jamii FM

Wazee kuhamasisha amani uchaguzi serikali za mitaa mkoani Mtwara

10 October 2024, 23:10 pm

Meja Mstaafu Mohamedi Mbwana akizungumza katika mkutano uliofanyia katika ukumbi wa Boma uliopo katia ofsi za mkuu wa mkoa wa Mtwara juu ya kuhamasisha vijana kuwa na uchaguzi wa amani na usalama(Picha na Musa Mtepa)

Dhamira ni kuwataka wazee kukaa na vijana na kuzungumzia suala la amani na usalama wa mkoa katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ,uchaguzi ambao umekuwa ukishuhudia heka heka za hapa na pale za vyama vya siasa.

Na Musa Mtepa

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Kanali Patrick Sawala, ametoa wito kwa wazee wa mkoa huo kuzungumza na vijana ili kupunguza mivutano inayoweza kujitokeza kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika tarehe 27 Novemba 2024.

 Akizungumza katika mkutano na wazee Leo October 10, 2024, Kanali Sawala amesisitiza umuhimu wa kutumia lugha za staha ili kuwasaidia vijana kustahimiliana na kuweka amani.

Sauti ya Kanali Patrick Sawala mkuu wa mkoa wa Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala akizungumza na Wazee mkoani Mtwara(Picha na Musa Mtepa)

Kanali Sawala pia amewataka wazee kuhamasisha vijana kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo huku akisisitiza kuwa ni muhimu kuchagua viongozi walio na uwezo wa kuleta maendeleo kwa jamii.

Sauti ya Kanali Patrick Sawala mkuu wa mkoa wa Mtwara.

Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa Mkoa wa Mtwara, Meja Mstaafu Mohamedi Bakari Mbwana, amepongeza wito huo na kusema wapo tayari kuwasilisha ujumbe kwa vijana ili kuhakikisha wanashiriki kwa amani katika uchaguzi.

Sauti ya Meja mstaafu Mohamedi Bakari Mbwana mwenyekiti wa baraza la wazee mkoa wa Mtwara.
Baadhi ya wazee waliohudhuria kikao cha mkuu wa mkoa wa Mtwara wakiwa makini kusikiliza hotuba ya mkuu wa mkoa wa Mtwara(Picha na Musa Mtepa)

Mkutano huu umeonekana kama hatua muhimu katika kuhakikisha uchaguzi ujao unafanyika kwa amani na utulivu.