Jamii FM

TANECU kuwakomboa wakulima wa korosho Mtwara

3 October 2024, 12:48 pm

Wakulima wa zao la korosho wilaya ya Newala na Tandanhimba wakiwa kwenye mkutano wa ufunguzi wa kiwanda cha kubangua korosho kilichojengwa na TANECU (Picha na Musa Mtepa)

Kiwanda hiki kinakadiriwa kuwa na thamani ya shilingi bilioni 3.4 huku kikitarajiwa kubangua tani 3,500 za korosho kwa mwaka.

Na Musa Mtepa

Wakulima wa korosho katika wilaya za Tandahimba na Newala mkoani Mtwara wameonesha furaha yao kuhusu ujenzi wa kiwanda cha kubangua korosho kilichojengwa na Chama Kikuu cha Ushirika TANECU LTD katika kijiji cha Mmovo.

Wakulima hawa wamesema uwepo wa kiwanda hicho unawapa matumaini makubwa na usalama katika kutimiza malengo yao ya kiuchumi kupitia zao la korosho.

Sauti ya wakulima wa zao la korosho katika wilaya za Tandahimba na Newala
Mwenyekiti wa TANECU Karim Chipola akizungumza na waandishi wa habari siku ya uzinduzi wa kiwanda cha kubangua korosho(picha na Musa Mtepa)

Halima Salumu Mtale, mkazi wa Newala na msimamizi wa shughuli za ubanguaji, amesema kiwanda  kitawasaidia akina mama kiuchumi kwa kuwapa uwezo wa kujikimu na kugharamia mahitaji kama vile kulipa kodi na kusomesha watoto.

Sauti ya Halima Mtale msimamizi wa ubanguaji kiwandani hapo

Mwenyekiti wa TANECU, Karim Chipola, ameishukuru serikali kwa kusaidia ujenzi wa kiwanda hiki na kuwashauri wakulima wa Tandahimba na Newala kuwa na matumaini, hasa baada ya changamoto ya miaka mitatu iliyopita ya kupungua kwa bei ya korosho sokoni.

Sauti ya Karim Chipola mwenyekiti wa TANECU

Aidha, Chipola amesema wamejipanga kuhakikisha wanakuwa na masoko ya uhakika kwa korosho  karanga, ndani na nje ya nchi.

Sauti ya 2 Karim Chipola mwenyekiti wa TANECU

Chama Kikuu cha Ushirika TANECU LTD kinahudumia wakulima wa wilaya hizi na kina malengo ya kujenga viwanda 10 kwa kila wilaya, ili kuboresha thamani ya zao la korosho na kuwaa na manufaa kwa wakulima.