Jamii FM

Wasimamizi wasaidizi Mtwara DC wafundwa uchaguzi serikali za mitaa

30 September 2024, 14:58 pm

Wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata na vijiji wa halmashauri ya Mtwara vijijini wakipata mafunzo ya uchaguzi wa serikali za mitaa (picha na Musa Mtepa)

Haya yote ni katika kuhakikisha elimu inawafikia makundi ya aina mbalimbali kuhusiana na uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwezesha kupata viongozi waliokidhi vigezo,kanuni na masharti yaliyolengwa .

Na Musa Mtepa

Ndug. Abeid Abeid Kafunda, msimamizi wa uchaguzi, amesisitiza umuhimu wa kufuata taratibu na kanuni ili kuepusha sintofahamu zinazoweza kujitokeza katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika November 27,2024.

Wito huo ametolewa leo September 30,2024 wakati wa ufunguzi wa semina uliofanyika kwenye shule ya sekondari Mustafa Sabodo.

Kafunda amewataka wasimamizi wasaidizi wa ngazi ya kata na vijiji kuwa makini na kuzingatia mafunzo watakayopatiwa.

Sauti ya Abeid Abeid Kafunda msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Mtwara vijijini.
Msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Mtwara dc Abeid Kafunda akizungumza na wasimamizi wasaidi ngazi ya kijiji na kata katika mafunzo yaliyofanyika leo september 30,2024(Picha na Musa Mtepa)

Shamimu Heri, msimamizi msaidizi wa uchaguzi kata ya Mayanga, ameeleza kuwa mafunzo hayo yatawasaidia kusimamia uchaguzi kwa haki na uhuru ili kupata viongozi watakaokidhi vigezo.

Sauti ya Shamimu Heri msimamizi wa uchaguzi msaidiz ngazi ya kata ,kata ya Mayanga.

 Pia, Jasmini Liwowa na Idrisa Asali, wasimamizi wa ngazi ya vijiji, wamesisitiza kuwa mafunzo hayo yatasaidia katika hatua zote za uchaguzi, kuanzia kwenye kujiandikisha kwa wapiga kura hadi kwenye zoezi zima la uchaguzi.

Sauti ya Jasmini Liwowa na Idrisa Asali wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya vijiji.

Mafunzo haya ni muhimu katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa ufanisi na kwa kufuata sheria.