Jamii FM

Kafunda Ataka Uelewa Kanuni za Uchaguzi Mtwara Vijijini

29 September 2024, 00:35 am

Wawakilishi wa makundi mbalimbali wakisikiliza maelekezo ya uchaguzi wa serikali za mitaa kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi Mtwara vijijini(Picha na Musa Mtepa)

Kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa serikali imejikita katika kuhakikisha inatoa elimu ya kutosha kwa wananchi wote wenye sifa wanashiriki kikamilifu katika uchaguzi huo kwa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali ili waweze kushiriki katika kuchagua kiongozi wanae mtaka

Na Musa Mtepa

Msimamizi wa uchaguzi katika Halmashauri ya Mtwara Vijijini, Abeid Abeid Kafunda, amezungumza na makundi mbalimbali kuhusu uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024. Katika mazungumzo yake, Kafunda amesisitiza umuhimu wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu kanuni na sifa zinazohitajika kwa wagombea na wapiga kura.

Sauti ya 1 Abeid Abeid Kafunda msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Mtwara Vijijini.
Msimamizi wa uchaguzi katika halmashauri ya Mtwara vijijini Abeid Kafunda akitoa maelekezo ya uchaguzi kwa makundi mbalimbali yaliyojitokeza ofisini kwake ikiwa kama njia ya kujengab uelewa juu yakanuni na taratibu za uchaguzi wa serikali za mitaa (Picha na Musa Mtepa)

Kafunda amewakumbusha wajibu wa makundi hayo kuwa na utaratibu katika shughuli zao na kuendelea kuelimisha vijana na jamii kuhusu taratibu za uchaguzi.

Sauti ya 1 Abeid Abeid Kafunda msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Mtwara Vijijini.

Viongozi wa dini na wazee kutoka kijiji cha Msangamkuu wameeleza kuridhishwa na juhudi za serikali katika kuwajengea uelewa  huku wakiahidi kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa uchaguzi.

Sauti ya viongozi wa dini,Wazee na wawakilishi wa NG’OS

Makundi yaliyoshiriki ni pamoja na vijana, watu wenye ulemavu, viongozi wa dini, wazee wa kimila, na asasi za kiraia, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kufikisha elimu kwa jamii nzima.