Dkt. Biteko azitaka halmashauri kutumia fedha za gesi kubadilisha maisha ya wananchi
11 September 2024, 08:43 am
Halmashauri zilizopo kwenye miradi ya uchimbaji wa Gesi Asilia zihakikishe fedha za ushuru zina wanufaisha wananchi wa maeneo husika na sio kama hali ilivyo hivi sasa.
Na Musa Mtepa
Naibu waziri mkuu na waziri wa nishati Dkt Dotto Biteko ameziagiza halmashauri zilizopo katika miradi ya Gesi kutumia fedha zitokanazo na ushuru wa uchimbaji wa gesi asilia ili kubadili maisha ya wananchi wa maeneo hayo badala ya kusubiri bajeti kutoka serikali kuu.
Dkt Biteko ametoa agizo hilo September 11, 2024 katika kijiji cha Nanguruwe mkoani Mtwara katika hafla ya kukabidhi leseni ya uendelezaji eneo la ugunduzi wa Gasi Asilia la Ntorya.
Sambaba na hilo Dkt Biteko ametoa wito kwa kampuni ya ARA Petroleum na Ndovu kuwapa kipaumbele wakazi wa eneo la mradi utoaji wa ajira ili kutengeneza muunganiko wa wananchi na uchumi wa maeneo hayo.
kwa upande wao wakazi wa eneo hilo wameoneshwa kufurahia na ujio wa waziri huyo huku wakiiomba serikali kuwalipa stahiki zao kwa wakati ili kuondoa usumbufu baina yao.
Mara ya mwisho kwa serikali kutoa leseni ya uendelezaji wa visima vya gesi ilikuwa mwaka 2006.