Jamii FM

Wananchi Msimbati wafurahia ujenzi wa kituo cha afya

10 September 2024, 08:18 am

Mwonekano wa baadhi ya majengo ya kituo cha afya Msimabati (Picha na Musa Mtepa)

Ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji cha Mtandi kata ya Msimbati ni katika kutekeleza maagizo yaliyotolewa na naibu Waziri mkuu na waziri wa nishati DK Dotto Biteko alipofanya ziara katika eneo na kutoa maagizo ya kuwajengea kituo cha afya,kituo cha Polisi ,taa za Barabarani kupitia fedha za mrejesho wa jamii (CSR) zinazptokana na uzalishaji wa Gesi Asilia katika eneo hilo.

Na Musa Mtepa

Wananchi wa kata ya Msimbati wameishukuru serikali kwa kitendo cha kuwajengea kituo cha afya kitakachosaidia kupunguza baadhi ya gharama walizokuwa wanazitumia  kuzifuata huduma za afya umbali umrefu.

Wananchi hao wamesema  kuwa huduma za afya za uhakika wanazipata katika hospitali ya mkoa ya Ligula ambayo ipo umbali mrefu kutoka katika Kijiji hicho.

Sauti ya wananchi wa kata ya Msimbati wakizungumzia
Baadhi ya majengo ya kituo cha Afya Msimbati (Picha na Musa Mtepa)

Naye Mbunge wa jimbo la Mtwara vijijini Mh Shemsia Mtamba ameishukuru serikali kwa kusikiliza kilio cha wakazi wa kata ya Msimbati  kwa kuwajengea kituo hicho afya na kumuomba naibu Waziri wa nishati Judith Kapinga kupeleka shukrani hizo kwa Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassani.

Sauti ya Shemsia Aziz Mtamba Mbunge wa Jimbo la Mtwara vijijini

Akizungumza na Wananchi wa Msimbati Naibu Waziri wa Nishati amesema kuwa hadi kufikia September 30,2024 kituo hicho kitakuwa kimekamilika na tayari kwa kuanza kutoa huduma.

Sauti ya Judith Kapinga Naibu Waziri wa nishati
Mwonekano wa kituo cha Polisi Msimbati (Picha na Musa Mtepa)