Jamii FM

Madiwani halmashauri ya Kilindi wajifunza uzalishaji wa Korosho TARI Naliendele

13 June 2024, 19:00 pm

Mtaalamu wa zao la Korosho kutoka kituo cha utafiti wa kilimo TARI Naliendele Dr Fortunus Kapinga akiwapa maelekezo kamati ya fedha na mipango kutoka halmashauri ya Kilindi waliofika kituoni hapo kujionea jinsi na namna miche inavyozalishwa pamoja na namna ya kupambana na magonjwa (Picha na Musa Mtepa)

Baada ya kikao kilichoagiza kila halmashauri kuwa na vyanzo vipya vya mapato halmashauri ya Kilindi ilifikiria kuwa zao la korosho linaweza kuwa chanzo sahihi cha kuongeza mapato kwa siku za usoni hasa hamasa ikitolewa kwa wananchi na ukizingatia kuna misitu mingi ambayo haijafanyiwa kazi.

Na Musa Mtepa

Kamati ya fedha, Uongozi na Mipango ya halmashauri ya wilaya ya kilindi mkoani Tanga Juni 12,2024 wamefanya ziara ya siku moja katika kituo cha utafiti wa kilimo (TARI) Naliendele kujifunza taratibu za Miche na Mbegu ,Ubora na Magonjwa yanayoweza kukabiri zao la korosho na namna ya kuyaondoa.

Akizungumza baada ya ziara hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kilindi Idrisa Omari Mgaza amesema wamefika mkoani Mtwara kwa dhamira ya kujifunza juu ya kilimo cha zao la Korosho ikiwa ni moja ya  mpango wa kuongeza mapato ya halmashauri kupitia zao hilo .

Sauti ya 1 Idrisa Mgaza mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilindi mkoani Tanga

 Aidha Mh Mgaza amesema mkoa wa Tanga wanalima Korosho ila  sio kwa kiwango kikubwa kama ilivyo katika mkoa wa Mtwara na wao kama halmashauri kwa mwaka huu wakitarajia  kuanzia kulima hekari 400 za Mikorosho.

Sauti ya 2 Idrisa Mgaza Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.

Seiya Keiya na Michael Yeyo wajumbe wa kamati ya fedha ,uongozi  na mipango kutoka halmashauri ya Kilindi wamesema ziara hiyo ni mojawapo ya kutekeleza maagizo ya serikali ya kuhakikisha kila halmashauri kuwa na vyanzo vipya vya mapato .

Sauti ya Seiya Keiya na Michael Yeyo wajumbe wa kamati ya fedha,uongozi na mipango kutoka halmashauri ya wilaya ya Kilindi mkoani Tanga.
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya kilindi Mh Seiya Keiya akizungumza na Waandishi wa habari dhamira ya kutembelea mkoa wa Mtwara na sababu ya kujifunza uzalishaji wa zao la Korosho (Picha na Musa Mtepa)

Akimwakilisha mkurugenzi mtendaji  mkuu wa Idara ya kilimo, Mifugo na uvuvi wa halmashauri ya Kilindi Godian Gwiago amesema wamekuwa wakihangaika kwa muda mrefu katika kuongeza mapato ya halmashauri hivyo baada ya kushauriana kupitia baraza la Madiwani wakapitisha rasmi kilimo cha zao la korosho ili litumike kuongeza mapato hayo kwa siku za usoni.

Sauti ya Godian Gwiago mkuu wa Idara ya kilimo ,mifugo na uvuvi kutoka halmashauri ya Kilindi mkoani Tanga.

Kwa upande wake Bakari Kidunda mtafiti ambae pia kaimu mkurugenzi wa kituo cha utafit wa kilimo TARI Naliendele amesema dhamira kubwa ya ujio wao ni kujifunza na kupata uelewa juu ya kilimo bora cha zao la korosho Pamoja na fursa zake

Sauti ya 1 Bakari Kidunda mtafiti na pia ni kaimu mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa kilimo (TARI)Naliendele

Pamoja na hayo kaimu Mkurugenzi ameelezea sababu zinazosababisha kutembelewa na wageni kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya nchi kuwa ni Pamoja na kuwepo kwa watafiti wenye ujuzi na kujitangaza kazi zinazofanyika kituoni hapo .

Sauti ya 2 Bakari Kidunda Mtafiti na pia kaimu mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa kilimo (TARI) Naliendele.