Jamii FM

Wakulima wa mwani, wavuvi Mtwara waingia mgogoro

5 June 2024, 17:17 pm

Wakulima wa zao la mwani wakivuna na kuweka sawa kwa ajili ya kwenda kuukausha juani tayari kwa matumizi mbalimbali(Picha kwa hisani na Mtandao)

Kwa kawaida zao la mwani ni kivutio cha samaki kutoka maji mengi na kufika kwenye maji madogo kwa ajili ya kupata chakula, makazi na wakati mwingine kuzaliana. .

Na Musa Mtepa

Katika hali isiyotarajiwa wakulima wa mwani kutoka vijiji vya Namela na Msangamkuu Halmashauri ya Mtwara Vijijini mkoani Mtwara wamejikuta wakiingia katika mgogoro  na wavuvi   baada ya mashamba ya mwani kugeuka kuwa makazi na kivutio cha samaki .

Wakizungumza na Jamii FM redio wakulima hao wamesema kuwa miaka ya hivi karibuni vijiji vilivyopo ukanda wa pwani wa Mtwara hususani Msangamkuu walianzisha kilimo cha mwani kwa lengo la kuuza na kuongeza kipato cha familia ila kwa hivi sasa imekuwa na matarajio tofauti.

Hassan Mkama ni mkazi wa Msangamkuu na mkulima wa zao la Mwani amesema kuwa kilimo cha mwani kinaweza kuwa msaada mkubwa wa kurejesha uoto wa asili baharini na kuvutia upatikanaji wa Samaki kwa uwingi.

Sauti ya Hassan Mkama mkulima wa zao la mwani kutoka Kijiji cha Msangamkuu

 Naye Maafudhi Ally Ahmadi katibu msaidizi wa umoja wa usimamizi wa rasilimali Bahari (BMU)kijiji cha Namela na Bi Saada Abdalah wamesema wao ndio walikuwa waanzilishi wa zao hilo wamekuwa wakikutana na changamoto kutoka kwa wavuvi ambao wamekuwa wakifanya shughuli za uvuvi katika mashamba yao kwa kufuata Samaki wanaoishi katika mashamba hayo.

Sauti ya Maafudhi Ally Ahmadi katibu msaidizi wa BMU kijiji cha Namela na Bi Saada Abdalah mkulima wa Mwani kutoka Kijiji cha Namela.
Mwonekano wa shamba la Mwani (Picha kwa hisani ya Mtandao)

Kwa upande wake mzee Yusuf Ame na Selemani Mtandasa wavuvi wa Samaki kutoka kijiji cha Msangamkuu wanakili kuwa Samaki wanapatikana kwa uwingi kwenye mashamba ya Mwani kwakuwa ni sehemu rafiki kwao.

Sauti ya wavuvi wa Samaki kutoka kijiji cha Msangamkuu

Aidha kwa upande wake mtendaji wa kijiji cha Namela Bi Latifa Abilahi Malange amekiri kuwepo kwa mgogoro baina ya wavuvi na wakulima wa zao la Mwani huku hatua alizozichukua ni kuwaita wavuvi wanaoshutumiwa kufanya shughuli za uvuvi kwenye mashamba ya Mwani.

Sauti ya Bi Latifa Abila Mtendaji wa Kijiji cha Msangamkuu.