Jamii FM

Baraza la madiwani Mtwara labatilisha umiliki wa kiwanja cha Mbunge

24 May 2024, 23:15 pm

Waheshimiwa madiwani wa Manispaa ya Mtwara Mikindani wakizipitia taarifa mbalimbali za halmashauri robo ya tatu kilichofanyika leo 24/5/2024(Picha na Musa Mtepa)

Waheshimiwa Madiwani wameunga mkono kubatirishwa kwa kiwanja kinachosadikiwa kumilikiwa na Mbunge wa Mtwara Mjini huku mstahiki Meya akiwaagiza watendaji kuyatambua na kuyawekea alama maeneo yote yaliyopo chini ya halmashauri ili kurahisiasha utambuzi inapotokea mtu kuvamia maeneo hayo

Na Musa Mtepa

Baraza la madiwa  Manispaa ya Mtwara Mikindani limebatilisha uhalali wa umiliki wa kiwanja katika eneo la Shangani mashariki kinachosadikika kumilikiwa na Mbunge wa Mtwara Mjini baada ya kamati ya kudumu ya mipango miji,Ardhi na ujenzi kujiridhisha kuwa eneo hilo kuwa ni mali ya halmashauri.

Akitoa maagizo kwa Mkurugenzi mtendaji na watendaji wa halmashauri kupitia baraza la madiwa lililofanyika   leo tarehe 24/5/2024 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani  Mh. Shadida Ndile amesema kuwa maeneo yote ya halmashauri yatambulike na kuwekewa alama zinazojulikana ili kama kuna mtu anataka kuchukua eneo kinyume na taratibu aweze kutambulika

Sauti ya Shadida Ndile Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani
Mh.Shadida Ndile Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani akiongoza mkutano wa baraza la madiwani liliofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo(Picha na Musa Mtepa)

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya mipango miji,ardhi  na ujenzi ya manispaa ya Mtwara Mikindani ambae pia ni Diwani wa kata ya Naliendele Mh. Masudi Dali amesema baada ya kupitia katika vikao vya kamati juu ya uhalali na historia  waligundua kuwa mmiliki wa eneo hilo hajafuata utaratibu wa umiliki na kuliomba baraza kubatilisha umiliki wake.

Sauti ya Masudi Dali Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya mipango miji na ujenzi Manispaa ya Mtwara Mikindani.
Mh.Masudi Dali Diwani wa kata ya Naliendele ambae pia ni mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya mipangomiji,ardhi na ujenzi akitolea ufafanuzi juu ya kiwanja kilicho rudishiwa umiliki halmashauri(picha na Musa Mtepa)

 Naye Diwani wa kata ya Vigaeni Manispaa ya Mtwara Mikindani Mh Saidi Ali Nassoro(White) amesema kuwa  halmashuri ya Manispaa ya Mtwara mikindani lilipima eneo la Shangani kuanzia mwaka 1985 na eneo hilo liliachwa kwa ajili ya matumizi ya serikali na sio mtu binafsi.

Sauti ya Mh. Saidi Nassoro Diwani wa kata ya Vigaeni Manispaa ya Mtwara Mikindani
Mh.Saidi Nassoro Diwani wa kata ya Vigaeni Manispaa ya Mtwara Mikindani akichangia hoja ya ufutwaji wa umiliki wa kiwanja baada ya kujiridhisha kuwa ni mali halali ya halmashauri baada ya kamati ya mipango miji kujiridhisha(Picha na Musa Mtepa)

Abuu Mohamedi Abdala ni Diwani wa kata ya Shangani  ambae pia ni mjumbe wa kamati ya kudumu ya mipango miji, ardhi na ujenzi amesema kuwa baraza imetoa maamuzi ya kukifutia hati kiwanja hicho kwasababu ya taratibu za kawaida hazikufuatwa ikiwemo  mwombaji kuomba kumilikishwa na halmashauri kwakuwa lilikuwa linamilikiwa na mjomba wake .

Sauti ya Abuu Mohamedi Abdala Diwani wa kata ya Shangani Manispaa ya Mtwara Mikindani