Mila, desturi katika jando na unyago kwa watoto Mtwara
31 December 2024, 14:25 pm
Na Mwanahamisi Chikambu na Gregory Millanzi
Jando na Unyago ni mila na desturi muhimu zinazopatikana katika jamii nyingi za Tanzania na Afrika Mashariki. Sherehe hizi za mpito ni sehemu ya mchakato wa kuwafunda vijana wanaoingia utu uzima.
Jando:
Sherehe hii inalenga wavulana na mara nyingi huambatana na tohara pamoja na mafunzo ya kijamii na kiroho. Wavulana hufundishwa majukumu yao kama wanaume katika jamii, tabia njema, na mbinu za kujitegemea.
Unyago:
Kwa upande wa wasichana, Unyago ni sherehe inayolenga kuwapa mafunzo kuhusu afya ya uzazi, majukumu ya kifamilia, na jinsi ya kujiheshimu pamoja na kuheshimu wengine.
Katika makala haya, utawasikia makungwi kutoka mkoani Mtwara, Afisa Utamaduni wa Mkoa, na Mkurugenzi wa Shirika la SDA, Thea Swai, wakielezea umuhimu wa kuwajengea uwezo makungwi.