Jamii FM

 NSSF yadai zaidi ya bilioni 3.2  kwa waajiri mkoani Mtwara

31 May 2024, 12:49 pm

Bw Rebule Maira Meneja wa NSSF mkoa wa Mtwara akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake (Picha na Musa Mtepa)

Ndani ya mkoa wa Mtwara kuna deni lisilopungua takribani Bilioni 3.3 ambalo waajiri  29  bado hawajawasilisha michango yao kama inavyostahili na wakati mwingine hawataki hata kukaguliwa pale inapobidi kujua idadi ya wafanyakazi wao.

Na Musa Mtepa

Wajiri wametakiwa kutekeleza majukumu yao kwa asilimia mia moja kwa Wafanyakazi wao katika kuwaandikisha kama waajiriwa au Mwanachama wa mfuko  wa hifadhi ya jamii  ili watakapofika tamati ya ajira yao wapate mafao yaliyo mazuri na kwa wakati.

Hayo yamesemwa na Meneja wa mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) Mkoa wa Mtwara  Rebule Maira alipokuwa anazungumza na jamii fm redio ofisini kwake ambapo amesema kuwa kazi kubwa ya mfuko huo ni Pamoja na kusimamia waajiri kujiandikisha kama walipa michango na kusimamia ukusanyaji wa michango kutoka kwa mwajiri na mwajiriwa

Sauti ya 1 Bw Rebule Maira meneja wa NSSF mkoa wa Mtwara

Aidha Bw Rebule amesema, kuwa katika utekelezaji wa sheria na majukumu ya ukusanyaji michango wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali ikiwemo mwajiri kuficha kumbukumbu za  wafanyakazi na wakati mwingine kudanganya kiwango cha mshahara.

Sauti ya 2  Bw Rebule Maira meneja wa NSSF mkoa wa Mtwara

Pamoja na changamoto hizo Bw Rebule Maira amesema, wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali zikiwemo kumtembelea mwajiri kuzungumza nae ili kuona namna  anaweza kuwasilisha michango ya wafanyakazi wake.

Sauti ya 3 Bw Rebule Maira meneja wa NSSF mkoa wa Mtwara